Kishore Kumar Hits

Darassa - Shika текст песни

Исполнитель: Darassa

альбом: Shika


Abbah

Mguu pande, mguu sawa
Tembea, tembea
Nataka uwanja, nitambe
Sogea, sogea
Wako wapi wapambe?
Ooh, kapotea, kapotea
Ngoma isambe hiyo
Kidedea, kidedea
Masharti ya mganga wameyakosea
Wamekuja kuzima kumbe wanachochea
Wanaupepea moto, kolea, kolea
Mnadhani mimi ni wa kuchezea, chezea?
Zima redio mbao, haiya
Zima na mtandao, haiya
Sema nao, piga bao, haiya
Sisi sio sa-size yao, we
Vunja vigenge kimbiza mwenge kama desturi
Uso sawa wa kucheza, umevalia misuli
Utatumwagia radhi, utatuharibia shughuli
Miguu vizuri ulizia wananiitaga nguli
Kama unaimba, imba nikuitikie
Ngoma inanoga, kucheza mtu akupigie
Ucheke, ulie
Ishike, iachie
Mwenzangu niambie
Kaa chini ntulie
Shika, kamata, sukuma, twende
Shika, kamata, sukuma, twende
Shika, kamata, sukuma, twende
Shika, kamata, sukuma, twende
Shika (Shika), kamata (Kamata)
Shika (Shika), sukuma, twende
Shika (Shika), kamata (Kamata)
Shika (Shika), sukuma, twende

Mbuzi kafungwa kwenye chuma cha reli
Boss kaamka chumba cha uskeli
Bwana shamba, baiskeli vipi sheli?
Kiwanja hakiuzwi, ogopa matapeli
Ah, survivor kwenye jungle commando
Ukijijua panya ukatafute pango
Endelea endelea kushikia bango
Hatukuvui nguo, tunavua majigambo
Jembe la kulima, tifua, tifua
Navua papa itakua kamba, dagaa, kibua
Mshike, mshike segele langu unalijua
Ngoma inoge kelele zangu mpaka napasua
Panga, pangua
Ota, otea
Unataka? Chukua
Ngoja, ngojea
Tokea, sogea
Pokea, ongea
Usingoje usimuliwe una macho ya kujionea
Kama unaimba, imba nikuitikie
Ngoma inanoga, kucheza mtu akupigie
Ucheke, ulie
Ishike, iachie
Mwenzangu niambie
Kaa chini ntulie
Shika, kamata, sukuma, twende
Shika, kamata, sukuma, twende
Shika, kamata, sukuma, twende
Shika, kamata, sukuma, twende
Shika (Shika), kamata (Kamata)
Shika (Shika), sukuma, twende
Shika (Shika), kamata (Kamata)
Shika (Shika), sukuma, twende

Mbuzi kafungwa kwenye chuma cha reli
Boss kaamka chumba cha uskeli
Bwana shamba, baiskeli vipi sheli?
Kiwanja hakiuzwi, ogopa matapeli

Поcмотреть все песни артиста

Другие альбомы исполнителя

K.O

2021 · сингл

Похожие исполнители

Meddy

Исполнитель

Nandy

Исполнитель