Tulikotoka ni mbali Tukitazama nyuma Asingekuwa Bwana Tusingefika hapa Yale tuliyoyapitia Hayakutuacha tulivyo Haikuwa rahisi Ni mkono wa Bwana Mengine yalikuja kama mema Mwisho ukawa mbaya Mengine yalikuja kama mabaya Kumbe yanakusudi Lakini katika yote hayo Tulikuona Bwana Ukitetea maisha yetu Dhidi ya hatari mbaya Tulikutana na hatari mbaya Tukajua ni mwisho Tulikutana na majanga mengi Tukajua hakutakucha Lakini katika yote hayo Wewe ulisimama Kutetea maisha yetu Yasidhurumiwe Yah Yah Yah ayayaya Uuuuuuuh Kaa nasi Bwana Safari bado ndefu Tunakumbuka mengi Tuliyoyaona nyuma Tunakumbuka mengi Tuliyoyasikia Tulipitia magumu Yaliyotuchanganya sana Tulipitia mengi Yaliyotuvuruga mioyo Tunakumbuka ndugu zetu Tuliyowaacha nyuma huko Tulitamani leo hii Tungekuwa nao Uuuuuuuh Nakumbuka huyu alivyolia Eehh eehh Alipowakumbuka ndugu zake Eehh eehh Alitukaribisha kwao Ayayaya Akasema maneno haya Jamani karibuni nyumbani Hapa ndipo kwetu Kwanzia huku hadi kule Hizi ni nyumba zetu Na kama mnavyoona Wenyewe hawapo Nyumba imebaki kimya Na sisi tunaishi mbali Ayayayaya aya Mwingine alisimama Akatafakari Akapiga hesabu Za maisha yake Akaona mambo yake Hayako sawa Akatazama nyuma Alikotoka akasema Jamani niombeeni Mambo ni magumu Hali ninayopitia Hata sielewi Mwenzangu kabadilika Siyo kama zamani Hali inayoendelea Sijui itakwisha lini Ayayayaya Ni kweli tunapita Ni kweli yapo mengi Yanayotusibu Ila Mungu wetu Yuko palepale Ila wema wake Bwana Uko pale pale Katika yaleyale Wengine wanayolia sana Wapo wengine bado Wanaimarisha Katika yaleyale Yanayowatoa roho wengine Katika hayohayo wengine Wanasonga mbele Daudi anasema Katika magumu yote Nalimwona Bwana kasimama mbele yangu kumbe tatizo letu liko kwetu wenyewe tunaona magumu hatumuoni Bwana Tatizo haliko kwa Mungu Tatizo liko kwetu Wala haliko kwa shetani Tatizo liko kwetu Tatizo ni sisi wenyewe vile tunavyoona Hilo ndilo tatizo letu linalotusumbua Songa mbele Usitazame nyuma Mtazame Bwana Atakutia nguvu atakuinua na wewe usitazame nyuma mpendwa Mtazame Bwana