Kishore Kumar Hits

Pst. Faustin S. Munishi - Malebo текст песни

Исполнитель: Pst. Faustin S. Munishi

альбом: Namlilia Malebo, Vol. 6


Nina huzuni rohoni, mimi siimbi nalia
Namlilia Malebo amekataa kuokoka
Nilizoimba ni nyingi nikimuonya Malebo
Bado hajabadilika, sasa siimbi nalia
Yeye ni wangu rafiki tuliyesoma pamoja
Michezo ya utotoni tuliicheza pamoja
Sasa ni watu wazima na mimi nimeokoka
Malebo nikimwambia yeye anaruka kimanga
Si yeye peke yake ninao wengi rafiki
Niliwaimba kimbele kwenye kaseti ya pili
Wengine wamekubali wamemwamini Mwokozi
Yesu amewasamehe amebakia Malebo
Tangu zamani huwa akinitafuta
Aninunulie chang'aa, bangi, sigara na beer
Nikimwambia Malebo ninunulie chakula
Matusi tanitukana nimelalia maskio
Umenitusi malebo, uongo kuninenea
Mimi nimemsamehe najua tatizo lake
Yeye mtumwa wa dhambi anataka ukombozi
Mpaka atakapokubali Yesu atamkomboa
Nakuita Malebo uje kwa Yesu utubu
Yeye ni mwenye huruma atakusamehe kabisa
Jina lako la Malebo litaandikwa mbinguni
Utakuwa kiumbe kipya, ya kale yote tapita
Mkumbuke Mrefu alivyokuwa mbaya
Tangu alipokubali kumpa Yesu maisha
Ameshambadilisha sio Mrefu wa kale
Sasa anahubiri injili yake Mwokozi
Nawajua vizuri Pili na Tatu Pamoja
Walivyokuwa wakali watoto wa mtaani
Sasa wameshaokoka wamechanua vizuri
Wote wameokoka wana watoto nyumbani
Nimeshanawa mikono, damu yako sidaiwi
Yesu anayekupenda njoo kwake anakuita
Unanijua vizuri sina haja kueleza
Yesu 'linibadilisha na wewe 'takubadilisha
Anakuita ulivyo uje akubadilishe
Acha kutia mashaka anajua kazi yake
Kazi yako kuamini, kutubu makosa yako
Na yesu ni kusamehe na kukuosha kabisa
Hima njoo kwa haraka wacha kusita malebo
Ona ulivyo chakaa meno sita wametoa
Wale uliodanganya ukawaibia mapesa
Wengine washaapa watakungo'a mengine
Sio wote wapole kama unavyoniona
Pesa ulizonirusha mimi nimenyamaza kimya
Sasa wale wazaire uliowaibiwa madola
Wamesema wakikuona macho yako tayang'oa
Najua maskani unapoishi malebo
Jijini dar es salaam, keko ya magurumbasi
Pale mjini arusha huko unga limited
Na jiji la nairobi watakupata majengo
Kwote nimezunguka sijakuona kabisa
Wazazi wanisumbua hawakuoni nyumbani
Mkeo yule wa tano anakutaka nyumbani
Wale ulowafukuza wote pia wamerudi
Nakuita Malebo uje kwa Yesu utubu
Yeye ni mwenye huruma atakusamehe kabisa
Jina lako la Malebo litaandikwa mbinguni
Utakuwa kiumbe kipya, ya kale yote tapita

Поcмотреть все песни артиста

Другие альбомы исполнителя

Похожие исполнители