Tuma Baba tuma msaidizi x2 Tuma Yesu, tuma msaidizi x2 Yesu uliahidi wanafunzi wako Kwamba hautawaacha kama yatima Bali utawatumia msaidizi Awafunze, awape nguvu Awafariji mioyo Nami naja mbele zako Baba niko mbele zako Naomba unitumie msaidizi Anifunze, anipe nguvu Aniongoze kwa kazi yako Baba tuma msaidizi Tuma msaidizi Naomba Baba, nisaidie Nataka nguvu mpya Kila usiku ninapoenda kulala Nafungua bila mpango ukurasa wowote Ninasoma mistari michache tu naanza sinzia Nafunga Biblia naanza kuomba Kinachofuata naamka asubuhi kusema amina Baba nisaidie, Tuma nguvu zako, Tuma uwezo wako Tuma roho wako ndani yangu Baba (Refrain) Naomba, Nataka nguvu Baba mimi siwezi chochote bila wewe Naomba nguvu zako Baba (Refrain) Baba tuma, Nakuomba Baba, Tuma roho wako ndani yangu Anifunze, aniongoze, anitawale Mienenendo yangu aitawale Maombi yangu, kufunga kwangu aitawale Naomba tuma Baba Roho wako anifunze neno/ aombe/aimbe ndani yangu