Kishore Kumar Hits

Dully Sykes - Salome текст песни

Исполнитель: Dully Sykes

альбом: Dully Sykes Top Hits


Ohh
Oh, ohh
Salome juu ya kaburi lako nalia, haa!
Kilio nakisikia
Dakika za mwisho mpenzi wangu najutia, aah
Kosa nilokufanyia
Salome juu ya kaburi lako nalia, haa!
Kilio nakisikia
Dakika za mwisho mpenzi wangu najutia, aah
Kosa nilokufanyia
Siku ya kwanza nilikutana na wewe
Akili iliruka na kupata kiwewe
Sikuamini kama ningekutana na wewe
Hilo la kwanza naomba unielewe
Nikakutongoza ukanikubalia
Ulijipa moyo tena mia kwa mia
Umekwishapata bwana atakayekuoa
Kumbe nilikuona kama demu wa kuzugia
Miezi saba mbele iliendelea
Na mapenzi kwako we' yakapungua
Kumbe ulikuwa na mimba ya kujifungua
Miezi yote hiyo wala hukuniambia
Ulijua lazima nitaisaigia
Na ndio ndoto yangu hiyo ilikuwa
Na ulipojaribu mimi kuniambia
Katukatu nami nikakutalia
Salome mpenzi wangu ukaanza kulia
Kwa uoga wangu mimi nikakuambia
Tuonane siku inayofuatia
Kwa unyonge Salome ukaitikia
Salome juu ya kaburi lako nalia, haa!
Kilio nakisikia
Dakika za mwisho mpenzi wangu najutia, aah
Kosa nilokufanyia
Salome juu ya kaburi lako nalia, haa!
Kilio nakisikia
Dakika za mwisho mpenzi wangu najutia, aah
Kosa nilokufanyia
Siku ya pili tena ilipofikia
Asubuhi mapema mi' nikakimbia
Nikakimbia na kuelekea Mbeya
Huku nyuma Salome uliningojea
Saa, dakika, sekunde zilipotokea
Ulichoka mpenzi kwa kuningojea
Ikakubidi uje kuniulizia
Nyumbani wakesema Dully ameshakimbia
Salome mpenzi wangu ulinyong'onyea
Hazikupita dakika ukazimia
Ndoo za maji tatu wakakumwagia
Ndipo hapo fahamu zikakurudia
Ulilia mwishowe mpaka kujutia
Ulijuta kwa nini ulikunikubalia
Ulirudi nyumbani kwenu unalia
Hadi chumbani kwako ukajifungia
Salome mpenzi wangu ukaandika barua
"Msimfunge Dully, mimi najiua"
Dakika tano mbele zilipowadia
Polepole kitanzi ukajifungia
Ukajinyonga na kuiaga dunia
Nisamehe Salome leo najutia
Ukajinyonga na kuiaga dunia
Nisamehe Salome leo najutia
Salome juu ya kaburi lako nalia, haa!
Kilio nakisikia
Dakika za mwisho mpenzi wangu najutia, aah
Kosa nilokufanyia
Salome juu ya kaburi lako nalia, haa!
Kilio nakisikia
Dakika za mwisho mpenzi wangu najutia, aah
Kosa nilokufanyia
Salome juu ya kaburi lako nalia, haa!
Kilio nakisikia
Dakika za mwisho mpenzi wangu najutia, aah
Kosa nilokufanyia
Salome juu ya kaburi lako nalia, haa!
Kilio nakisikia
Dakika za mwisho mpenzi wangu najutia, aah
Kosa nilokufanyia
(Ha, Dully sykes, Mika Mwamba)

Поcмотреть все песни артиста

Другие альбомы исполнителя

Похожие исполнители

Chege

Исполнитель

Fid Q

Исполнитель

Wahu

Исполнитель