Kishore Kumar Hits

Goodluck Gozbert - Hauwezi Kushindana текст песни

Исполнитель: Goodluck Gozbert

альбом: Goodluck Gozbert


Hmm, halleluyah
(Produza Paulo)
Ah, ah, a-ya, ya-ya-ya
Hauwezi kushindana, oh kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa, a-ya, ya-ya-ya
Hauwezi kushindana oh kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa, a-ya, ya-ya-ya
Mm, kama maneno yangekuwa yanaweza kutoboa mwili huu
Mbona sasa ningekuwa na vidonda mwili mzima
Vita ya maneno kuna watu ni majemedari
Ukisema mshindane mbona mikono utainua
Kupigwa vita ni kawaida isikusumbue
Wewe ni muti wenye matunda zoea mawe
Lia kidogo nyamaza ili uchungu uishe
Ah, ukiendelea unawapa kichwa hao
Vaa silaha za imani rejea vitani
Wakikuona waseme umeshakua sugu (sugu)
Oh, acha waonge, acha waseme seme
Ila yupo Mungu wakuwaziba midomo
Hauwezi kushindana, oh kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa, a-ya, ya-ya-ya
Hauwezi kushindana oh kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa, a-ya, ya-ya-ya

Eh, ikiwa Mungu anahukumu kwa kus'kiza maneno
Mbona hata matumbo ya mimba yanasemwa sana (kazaliwa)
Hivi Mungu angehukumu kwa kus'kiza umbeya
Si' ningekushauri mchungaji wangu ufunge kanisa
Mwanadamu, mwanadamu, shida ni ulimi
Ungejifunza ukimya haunaga hasara
Fulani, we fulani unashida gani
Na uongo wa nini? Mwogope Mungu
Ukumbuke ni ahadi kuna siku yaja
Kwa kila neno la kinywa chako, utatolea hesabu
Mimi (mimi) si' nimeshakwambia kubali uache
Utajijua na shingo yako ngumu a-ya, ya-ya-ya
Siwezi kushindana, oh kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa a-ya, ya-ya-ya
Hauwezi kushindana (hauwezi), oh kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa, a-ya, ya-ya-ya
Hauwezi kushindana, oh kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa, a-ya, ya-ya-ya
Yesu huyu Yesu, hakujitetea kabisa
Japo walimsema kwa ubaya, aliwasamehe
Na wewe uwasamehe, uwaombee
Kwa maana hawajui wasemayo
Wakifanyanga ubaya (uwajibu kwa wema), oh
Usishindane na mtu (wajibu kwa wema)
Hata iwe ni ndugu wa karibu (wajibu kwa wema)
Si' vizuri wewe usilipe kisasi (wajibu kwa wema)
Tenda wema uende (wajibu kwa wema), eh
Ah-ah-ah (wajibu kwa wema), oh maana maana
Hauwezi kushindana (o-lolo), oh kushindana (oyo)
Na mwanadamu mwenye kinywa, a-ya, ya-ya-ya (ukisimama maneno yatosha)
Hauwezi kushindana oh kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa, a-ya, ya-ya-ya (wewe uliye mkuu)
Hauwezi kushindana (o-lolo), oh kushindana (eh-eh)
Na mwanadamu mwenye kinywa, a-ya, ya-ya-ya (watakupenda ukifa wewe)
Hauwezi kushindana (hauwezi) oh kushindana (wacha)
Na mwanadamu mwenye kinywa, a-ya, ya-ya-ya (kinywa)
(Maneno mtu humpangii nini aseme)

(Ahsante)

Поcмотреть все песни артиста

Другие альбомы исполнителя

Похожие исполнители