Tulifunga macho kuomba Tuliibiwa ardhi Bendera ya Mungu ilipeperuka Mwafrika akikaa kwa imani Cheupe kilijiuza Cheusi kilifukuzwa Tuliambiwa, 'Imbeni alleluia, Fungeni macho imbeni.' Tumegongwa tumeamka Tumekanyagwa tumejitoa Tumelazwa tumesimama heye! Tumebanwa tumeepuka Kusulubiwa tumeshuka Tumeuawa tumefufuka aye! Mwaka wa 1963 Tulijishindia Uhuru Bendera ya Mzungu iliteremshwa Mwafrika alianza kujitawala Tuliambiwa, 'Harambee! Harambee! Vuruteni mzigo.' Tuliambiwa Fuata Nyayo! Fungeni macho fuata Nyayo! Tumegongwa tumeamka Tumekanyagwa tumejitoa Tumelazwa tumesimama heye! Tumebanwa tumeepuka Kusulubiwa tumeshuka Tumeuawa tumefufuka aye! Machozi ya mKenya inagonga mchanga wa Afrika kama laana Damu-victims kosana Colonization aftermath ya urbanization Matokeo ghetto kibao zenye homeless, landless Merciless, visionless leaders Kuendeleza nepotism, tribal clashes, capitalism Division ya social classes Division from Runda to Kibera, Kileleshwa to Dandora Tulisahau rangi za bendera History, haki na Ukweli Swali. Mtumwa wa kiakili unaenda wapi kama umefunga macho? Juu yako na vizazi vijavyo Hurry mKenya Kuamka au kutoamka Kilio cha Mama Afrika Kunajisiwa kisiasa. Na bado twangoja wokovu Twaangalia milimani Twauliza Mwokozi wa nani Twafaa kutazama kiooni Kila mmoja ni kiongozi Kila mmoja ni mwalimu Kila mmoja ni mjenzi Kila mmoja achukue madaraka Tumegongwa tumeamka Tumekanyagwa tumejitoa Tumelazwa tumesimama heye! Tumebanwa tumeepuka Kusulubiwa tumeshuka Tumeuawa tumefufuka aye! Tumegongwa tumeamka Tumekanyagwa tumejitoa Tumelazwa tumesimama heye! Tumebanwa tumeepuka Kusulubiwa tumeshuka Tumeuawa tumefufuka aye!