Kishore Kumar Hits

Kinondoni Revival Choir - Mtu Wa Nne текст песни

Исполнитель: Kinondoni Revival Choir

альбом: Mtu Wa Nne


Ni nani huyo,
Nimuonaye,
Mtu wa nne,
Ndani ya moto
(Ni nani eeh)
Ni nani huyo,
Nimuonaye,
Mtu wa nne,
Ndani ya moto,
Twamsoma Shadraki,
Meshaki, Abedineko,
Walipotupwa kwenye tanuru,
Ili wateketee,
Muujiza ukatokea,
Yesu kaingia humo,
Akawaficha na moto,
Haukuwaunguza,
(Ni nani eeh)
Ni nani huyo,
Nimuonaye,
Mtu wa nne,
Ndani ya moto
Ni nani huyo,
Nimuonaye,
Mtu wa nne,
Ndani ya moto,
Na Nebukadineza, kashangaa,
Kawaita mawaziri, kauliza,
Je hatukuwatupa, watu watatu,
Mbona sasa ninaona, wako wanne
(Ni nani eeh)
Ni nani huyo,
Nimuonaye,
Mtu wa nne,
Ndani ya moto
Ni nani huyo,
Nimuonaye,
Mtu wa nne,
Ndani ya moto,
Haleluya!!
Naye ni nani atakaye washitaki,
Wateule wa Mungu Jehova,
Tena ni nani atakaye wahukumu,
Wateule wa Mungu Jehova,
Bali Mungu mwenyewe huwalinda,
Tena Mungu mweyewe huwatetea,
Bali Mungu mwenyewe huwalinda,
Tena Mungu mweyewe huwatetea
(Ni nani eeh)
Ni nani huyo,
Nimuonaye,
Mtu wa nne,
Ndani ya moto
Ni nani huyo,
Nimuonaye,
Mtu wa nne,
Ndani ya moto,
Itakuwa kwako, mtu wa Mungu,
Ukijaribiwa na mwovu,
Yesu atakuja, vumilia,
Kwenye shida yako, kukuponya,
Itakuwa kwako, mtu wa Mungu,
Ukijaribiwa, na mwovu
Yesu atakuja, usihofu,
Kwenye shida yako, kukuponya,
Watashangaa, waliokushitaki,
Wataulizana, imekuwaje,
Watashangaa, walokutegea,
Wataulizana, nani kamuokoa,
Watashangaa, waliokushitaki,
Wataulizana, imekuaje,
Watashangaa, waliokutegea,
Wataulizana nani, kamuokoa,
Nawe utasema, ni Yesu,
Halleluyah!!!
Tena utasema, ni Yesu,
Eeh
Ni Yesu, amenitendea,
(Aah ni Yesu eeh)
Ni Yesu amenitendea,
(Yeye Bwana ananipenda sana, halleluyah)
Ni Yesu amenitendea,
(Yeye Bwana ananijali mimi, halleluyah)
Ni Yesu amenitendea,
(Yeye ndiye mlinzi wangu Bwana, halleluyah)
Ni Yesu amenitendea
(Yeye ndiye mtetezi wangu Bwana, halleluyah)
Ni Yesu amenitendea...
(Nataka niseme na wewe uliye kata tamaa
Inawezekana umetupwa Kwenye tanuru la moto
Naomba uvutie moyo Yesu ambaye ni mtu wa nne
Yuko pamoja nawe na atakwenda kukuinia tena halleluyah)
Amen
(Wewe mjane uliye nyimwa haki yako
Usiogope maana Mungu aliye Mme wa wajane yuko pamoja nawe
Na atakurejeshea yale yote uliyopoteza sema amen)
Amen
(Wewe yatima Mungu anakupenda
Hata kama unajiona uko pekee yako
Lakini Mungu aliye Baba wa yatima yuko pamoja nawe
Usiogope maana atakutunza halleluyah
Uko muujiza kwa ajili yako Wewe usiye na kazi
Uko muujiza kwa ajili yako Wewe mama usiye na mtoto
Nasema uko muujiza wa uponyaji wa magonjwa yako
Uko muujiza kwa ajili ya masomo yako
Ndugu yangu uko muujiza kwa ajili yako
Maana yeye Yesu alichukia mateso yetu na taabu zetu
Pale msalabani na huzuni yako ameniona
Machozi yako ameyaona usiogope
Kama alivyowatetea Shadraki, Meshaki na Abedneko
Hata kwaja kwako leo sema Amen)
Amen
(Sema Amen)
Amen
(Hebu twaweza tukaimba pamoja
Ni Yesu amenitendea
Hata kama unaona giza lakini Mungu anatenda kitu kwa ajili yako)
(Ni yesu amenitendea aah ni Yesu eeh)
Ni yesu amenitendea
(Yesu anapigana na adui zako sasa, -- halleluyah)
Ni yesu amenitendea
(Usiogope maana yeye yuko pamoja nawe, halleluyah)
Ni yesu amenitendea
(Atakuuisha na kuku
Ni yesu amenitendea
(Ndiyo maana ninampenda Bwana, halleluyah)
Ni yesu amenitendea
(Ndiyo maana ninamwimbia yeye, halleluyah)
Ni yesu amenitendea
(Ndiyo maana ninamsifu Bwana, halleluyah)
Ni yesu amenitendea
(Ooh ni Yesu eeh, halleluyah)
Ni yesu amenitendea
(Aah a ni Yesu eeh, halleluyah aaaah)
Ni yesu amenitendea

Поcмотреть все песни артиста

Другие альбомы исполнителя

Похожие исполнители